Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichowakuta waamuzi wa Bongo AFCON

Nassor Hamduni Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchini, Nassor Hamduni.

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache tu tangu orodha ya waamuzi walioteuliwa kuanza maandalizi kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zitakazofanyika mapema mwakani, huku hakuna jina lolote la marefa kutoka Tanzania, limemfanya Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchini, Nassor Hamduni avunje ukimya fasta.

Hamduni ameamua kuvunja ukimya kutokana na shutuma na mijadala iliyoibuka kwenye mitandao ya kijamii tangu orodha hiyo ilipowekwa hadharani na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambapo bosi huyo wa waamuzi nchini aliwataka wadau wa soka nchini kuacha kutoa lawama kwao kwa kukosekana kwa waamuzi hao.

CAF ilitoa orodha ya jumla ya waamuzi 68 watakaochezesha fainali hizo, huku kukiwa hakuna hata mmoja aliyechaguliwa kutoka Tanzania na kuibuka kwa mashambulizi ya maneno mtandaoni na Hamduni alisema;

“Watu wanatakiwa kutambua ni suala la nafasi tu kwa sababu waamuzi wetu wamefanya vizuri ndio maana unaona wanateuliwa kuchezesha Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo tusiwe walalamikaji.”

Hamduni aliongeza katika michuano ya kimataifa wapo waamuzi watano waliochaguliwa ambao watatu wataenda Afrika Kusini na wawili kwenda Uganda hivyo kama wasingekuwa bora wasingeteuliwa pia.

Katika waamuzi walioteuliwa, Kenya imetoa wawili, Burundi ikitoa mmoja katika eneo la Afrika Mashariki, wasaidizi 33 na kwenye teknolojia ya msaidizi wa waamuzi (VAR) wakiteuliwa wanne (4).

Mwamuzi wa mwisho kushiriki Afcon nchini alikuwa ni Frank Komba aliyetumika katika fainali zile zilizofanyika Cameroon ambapo kwa mwakani Tanzania itashiriki tena kwa mara yake ya tatu michuano hiyo mikubwa Afrika baada ya kukata tiketi kutoka Kundi F ikiungana na Algeria iliyotoka nayo suluhu katika mechi ya mwisho ya kufuzu iliyopigwa kule ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: