Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichopo nyuma ya pazia kufeli kwa Mastaa Simba na Yanga

Victor Akpan Nnn.jpeg Kiungo wa Simba Victor Akpan

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa zamani wa Yanga anaeikipiga Mtibwa Sugar, Balama Mapinduzi ametaja siri ya mastaa wengi wazawa kushindwa kufanya vizuri wakipata nafasi ya kusajiliwa Simba na Yanga kuwa ni kutokuaminiwa na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kama kwenye timu walizotoka.

Balama ambaye alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Alliance FC na kufanikiwa kuitumikia msimu mmoja tu kutokana na kupata majeruhi amefunguka hayo baada ya kuachwa na timu hiyo na kujiunga na Mtibwa Sugar akiwa mchezaji huru.

Akizungumza Balama anasema;

“Hakuna mchezaji ambaye hapendi kuwa bora kila mmoja anatamani kuwa mkubwa kupitia timu kubwa pale anapopata nafasi ya kusajiliwa, ila mambo yanakuwa magumu ukifika muda wa kucheza ni nadra sana kuingia moja kwa moja kikosini ili kuonyesha kile ulichonacho,”

“Uwezo unakuwa upo shida ni kutoaminiwa kitu ambacho kinasababisha wachezaji wengi kujikuta wanarudi walikotoka shida ambayo imekuwa ikituumiza tulio wengi lakini naamini kama tungeaminiwa na kucheza mara kwa mara tungeikia malengo.”

Akizungumzia kutua kwake Mtibwa alisema ni sehemu sahihi, kwani amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu sababu ya majeraha, ila anaamini atakuwa mtamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live