Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichomponza Chama ni ukaidi wa maagizo ya Robertinho?

Chama X Robertinho Substution Kilichomponza Chama ni ukaidi wa maagizo ya Robertinho?

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: Deo Mwanasoka

Nimeona mjadlaa wengi wakimlaumu kocha Robertinho juu ya uamuzi wa kumtoa Clatous Chama mapema sana mchezoni.

Nimekumbuka simulizi ya kisa cha Thierry Henry na Pep Guardiola katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya kati ya Barcelona na Sporting Lisbon.

Barcelona wakiwa wanacheza mpira mwingi sana, Henry aliamua kukiuka maelekezo ya Pep na kuacha eneo lake alilopangwa na kuhamia upande mwingine wa uwanja.

Muda mchache tu baada ya kuhama aliwapatia Barcelona bao la kuongoza na yeye mwenyewe alihisi kama alikuwa na mchezo mzuri.

Baada ya kuendelea kucheza kwa jinsi alivoona yeye mwenyewe ni sawa, Pep alimtoa na kumuelekeza kwamba alikuwa anavuruga plan yake.

Sub yake ilifanyika dakika ya 45 ya mchezo na kumbuka TH14 alikuwa mshambuliaji kinara na staa wa Barca.

Henry akamalizia kwamba Guardiola akiwa na plan unapaswa kuisimamia mpaka mwisho.

Nimefikiria sababu gani inaweza kumfanya kocha amuondoe Chama uwanjani mapema dakika ya 32 timu ikiwa inasaka matokeo. Kama si sababu tofauti na injury basi huenda Chama hakutii mpango wa kocha.

Makocha wote wakubwa duniani wanataka mchezaji aheshimu mpango wake. Kama watapoteza basi kocha ataulizwa.

Robetinho ameonesha mamlaka! Na inapaswa kuwa hivyo siku zote. Mpango wa kocha unapaswa kuheshimiwa.

Chanzo: Deo Mwanasoka