Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichomng’oa Balama Coastal Union hiki hapa

Mapinduzi Balama Kipenseli Kilichomng’oa Balama Coastal Union hiki hapa

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha kwanza chini ya kocha David Ouma, kiungo Balama Mapinduzi ametimka Coastal Union Mwanaspoti imebaini sababu za kuondoka kwake kuwa ni mtonyo.

Kwa mujibu wa Ouma amesema alikuwa anamuhitaji kiungo huyo kikosini kwake baada ya kumtengeneza acheze vile alivyokuwa anataka lakini maslahi yamemng’oa.

“Balama nimemkuta kikosini na nimemtengeneza vizuri naamini kila mmoja alikuwa anapenda uchezaji wake lakini sikuwa na namna ya kumzuia kubaki kutokana na viongozi kushindwana naye kimaslahi;

“Ni mchezaji mzuri alikuwa na mchango mkubwa kikosini lakini kuondoka kwake hakutaondoa ubora eneo hilo tayari tumeongeza wachezaji wengine ambao naamini watafanya vizuri.” alisema.

Alisema anaimani kubwa na wachezaji alio waongeza kikosi na anaamini wataziba malengo ya walioondoka na kuipa timu matokeo mazuri wanayoyatarajia ili kumaliza msimu nafasi nzuri huku akikiri kuwa amefanya usajili kulingana na matakwa yake.

Chanzo: Mwanaspoti