Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichomliza Enzo baada ya kocha kumtoa katika dk31 Chelsea ikiiua Newcastle

Enzo X Poch Kilichomliza Enzo baada ya kocha kumtoa katika dk31 Chelsea ikiiua Newcastle

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Chelsea imetangulia nusu fainali ya Kombe la Carabao baada ya kuifunga Newcastle kwa penalti 4-2 katika mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1, huku moja ya mambo yaliyostua ni kiungo Enzo Fernandez kutolewa katika dakika ya 31 tu ya mchezo.

Ishu nzima ilikuwa hivi;

Wakati Chelsea ikiivaa Newcastle katika robo fainali ya Kombe la Carabao kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, wageni walifunga bao la kuongoza katika dakika ya 16. Baadaye, katika dakika ya 31, kocha Mauricio Pochettino akamtoa kiungo huyo mshindi wa Kombe la Dunia na nafasi yake akaingia mshambuliaji Armando Broja.

Wakati hapakuwa na taarifa ya kuumia kwa kiungo huyo wa zamani wa Benfica, ukweli umebainika kwamba Enzo alikuwa akijisikia vibaya wakati wa mechi hiyo hivyo Pochettino akaona ni vyema ampumzishe. Kocha huyo wa The Blues alithibitisha jambo hilo baada ya mechi, akisema: "Alijisikia mgonjwa. Hakujisikia vyema kabla ya mechi na alipoanza kucheza, haikwenda vyema. Akaomba tumpumzishe kwa sababu hakuwa akijisikia vyema."

KISA CHA MACHOZI

Enzo alipotolewa alienda moja kwa moja kwenye vyumba vya kuvalia akifuatana na kocha msaidizi Jesus Perez na watu wengine wa benchi la ufundi.

Mashabiki wengi wa Chelsea wakavumisha kwamba kiungo huyo amepata majeraha ya kutisha. Hata hivyo, hofu ya mashabiki wa Chelsea, haraka ikatulizwa.

Mechi ilipomalizika, Enzo alionekana akimwagikwa machozi, jambo linaloaminika ni kujisikia vibaya kwamba hakuweza kuwa sehemu ya kikosi kilichopata matokeo yao bora zaidi kufikia sasa msimu huu.

KITUO KIFUATACHO KWA CHELSEA?

Makosa ya Kieran Trippier katika dakika ya mwisho (90+2), yaliirudisha mchezo Chelsea baada ya Mykhailo Mudryk kusawazisha na mechi kuingia katika hatua ya matuta ambako The Blues ikashinda kwa penalti 4-2.

Chelsea mechi ijayo itakuwa ni ya Ligi Kuu England ugenini dhidi ya Wolves Jumapili.

MATOKEO MENGINE ROBO FAINALI CARABAO

Everton 1 – 1 Fulham

(Fulham imepita kwa penalti 7-6)

Port Vale 0 – 3 Middlesbrough

RATIBA LEO

ROBO FAINALI CARABAO

Liverpool v West Ham (saa 5:00 usiku)

Chanzo: Mwanaspoti