Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichomkuta Humoud kwenye Ligi ya Zambia

Hunud Kilichomkuta Humoud kwenye Ligi ya Zambia

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Konkola Blades FC, Mtanzania Abdulrahim Humoud, amezungumzia ushindani wa Ligi Kuu ya Zambia na namna unavyomsaidia kucheza kwa kiwango cha ushindani.

Humoud alisema ligi ya Zambia siyo nyepesi, kila timu inapambana kusaka matokeo ya ushindi, hivyo lazima kama mchezaji aonyeshe kiwango cha juu, kitakachompa heshima ya kuitwa mgeni.

"Soka la Zambia ni gumu, linachezwa kwa kasi na nguvu, wachezaji wengi wanaondoka kwenda kusaka fursa nchi nyingine, jambo ambalo ni zuri kwao,"alisema na kuongeza;

"Ukilinganisha na Ligi Kuu Bara ipo juu, ina mvuto kwa Afrika na ndio maana wageni ni wengi Tanzania na huku wanaizungumzia vizuri na kwa ukubwa, pia nadhani inatokana na Wazambia wanaocheza Bara wameonyesha kiwango kikubwa."

Alisema kama mchezaji wa kigeni zipo changamoto za hapa na pale, anazoweza kukutana nazo, ila haziwezi kumtoa kwenye mstari wa mapambano, badala yake anazipa uzito ndoto kuzitimiza.

"Maisha ni yale yale, ambayo mchezaji yoyote akiwa mgeni anaweza kukutana changamoto, lakini ukijua nini unafanya basi utaelekeza nguvu kwenye majukumu yako,"alisema.

Jambo lingine ambalo linampa nguvu na kutokukata tamaa alieleza kuwa "Nilichogundua kwenye maisha usikubali kukatishwa tamaaa, riski anatoa Mungu,ukipata nafasi ya kupambana pambana.

Baadhi ya timu alizozichezea ni Ashanti United (2007/08), Mtibwa Sugar (2008–2010), Simba (2010/2011), Azam FC (2011–2013), Simba(2013/2014), Sofapaka (2014), Coastal Union (2014–2016), Real Kings (2016/2017), Malindi (2017), KMC FC (2018), Arusha United (2018–2019), Mtibwa Sugar (2019).

Chanzo: Mwanaspoti