Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichoiponza Stars kwa Morocco ni hiki

Tanzania Morocco.jpeg Kilichoiponza Stars kwa Morocco ni hiki

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pamoja na kuwa Tanzania tumecheza na timu bora sana namba moja Barani Africa na kiukweli wamewekeza sana kwenye soka lao kuliko sisi lakini tumecheza hovyo sana.

Tumecheza chini ya kiwango, approach ya mwalimu Adel Amrouche ya mfumo wa 5-2-3 haikumlipa. Pamoja na kucheza watu 9 nyuma ya mpira kwenye low block lakini bado Moroccowameweza kuifungua deffensive zone yetu na kutengeneza nafasi za kutosha na kisha kuzitumia kuzalisha mabao ya kutosha.

Namna ambavyo tulikuwa tunacheza hapakuwa na pattern iliyotengenezwa bora ya ushambuliaji mbele kwenye eneo la 14 zones tulikuwa hatufiki mara nyingi waliweza kutu press kwa juu sana na kutokutupa nafasi ya kuingia kwenye eneo lao la 1/3 ya zone yao kirahisi na wakafanikiwa kwa hilo.

Kwangu mimi Mbwana Samatta hakupaswa kutoka isipokuwa alipaswa kuongezewa watu wa kucheza naye mechi ya leo ilikuwa inamuhusu sana Kibu Denis kwakuwa ana nguvu anaweza kukimbia sana na ana uwezo mkubwa wa kukaba.

Aishi manula anapaswa kubadilika aina yake ya uokoaji wa mipira wengi mnabisha juu ya hili kama mmemtazama vizuri anaokolea sana kwa kutemea mipira ndani kidogo azalishe goli lingine tena la aina hiyo hiyo ya kutemea ndani.

Baadhi ya wacheza wa Taifa stars wamekosa kabisa hali ya upambanaji na kuonekana hawana kabisa mpango kazi wakati timu ikiwa inacheza.

Mwalimu Adel Amrouche ana kazi kubwa sana ya kufanya kwa michezo iliyobakia ukizingatia Stars yupo kwenye kundi gumu sana.

Kadi nyekundu ya Novatus ilivuruga mpango wote wa mwalimu kujilinda, kucheza pungufu dhidi ya Morocco ilikuwa lazima tuadhibiwe hakuna kauli nyingine ya kusema.

Tujipange kwa ajili ya michezo ijayo lakini kama taifa kuna haja ya kuweka mpango mkakati madhubuti wa kutengeza Taifa Stars bora zaidi miaka ya hivi karibuni, vinginevyo tutaendelea kuwa wasindikizaji kila mwaka.

FT: MOROCCO 3 0 TANZANIA.

Maoni ya mdau wa soka Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live