Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila timu inataka kuwa kama Yanga

Yanga Kikosii Kila timu inataka kuwa kama Yanga

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga SC wana timu iliyokamilika sana, wanavutia mno,yeyote atakayepata nafasi atakiwasha vyema, soka linapigwa la viwango vya juu mno.

Tabora United wamekutana na Yanga SC wakati mbaya sana,mbinu na mikakati yao ilikuja kufeli kabisa kipindi cha pili, Gamondi aliingia na plans bora huku Yanga SC wakiwa makini kwenye matumizi sahihi ya nafasi (Umakini+Kasi).

Note:Maxi Nzengeli amechukua Tuzo ya Mchezaji bora wa Mchezo,amestahili tuzo hiyo kafanya kazi kubwa na nzuri, anakaba vyema, anatafuta mipira huku akiwa na kasi na utilivu wa kutosha kwenye kuichezesha timu huyu jana ndio alikua muhimili mkubwa kwa upande wa Yanga SC.

Kama Kibwana huyu ndio mkataba wake unaelekea ukingoni basi Yanga SC watakaa nae mezani haraka ni mlinzi mwenye uwezo na hari ya kutosha Uwanjani, jana kaja kivingine na kutengeneza bao moja.

Impiri Mbombo,kKama Tabora wangeweza kumtumia vyema basi angewapa kitu kikubwa ni winga mwenye kasi na maarifa makubwa alikosa wasaidizi sahihi wa kumtupia mipira vyema.

Najim pale katikati kafanya kazi nzuri, ni Kiungo mwenye muendelezo mkubwa kakutana na viungo wa daraja la juu lakini hawakuzuia kucheza vyema.

Pacome Zouzoua amejerea na kuweka pasi moja ya goli,Ubora ni ule uleee amerejea kwa speed ya 5G. Super Guede anaendelea kutupia mechi mfululizo tu, kasi yake inazidi kuongezeka.

Yanga SC wametinga Nusu Fainali ya CRDB FEDERETION CUP kwa ushindi wa magoli 3-0 mbele ya Tabora United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live