Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila timu ina mgawo wake Uefa msimu huu

UEFA Mgao Kila timu ina mgawo wake Uefa msimu huu

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu za Ligi Kuu England zinajiandaa kuvuta mkwanja mrefu kabla hata hazijagusa mpira kwenye michuano ya Ulaya msimu huu.

Kuna klabu saba za England kwenye michuano mitatu ya Uefa, ambayo itakuwa na mabadiliko makubwa kuanzia msimu huu.

Mfumo huo mpya utafanywa kwa kuiga mtindo wa ligi ya Uswisi, badala ya ule mtindo wa zamani wa kuwa na makundi manane yenye timu nne, ambao timu mbili za juu zilikuwa zinakata tiketi ya kufuzu hatua inayofuata.

Kabla hata michuano hiyo haijaanza, timu zitakazoshiriki kwenye michuano yote kuanzia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa League na Europa Conference League zitaweka kibindoni mkwanja wa maana kabisa.

Ushindi kwenye kila mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya unaweza kuifanya timu hiyo kuvuna mkwanja kati ya Pauni 140 milioni hadi Pauni 145 milioni.

Lakini, kabla hata mpira haujaguswa kwenye michuano hiyo ya Ulaya msimu huu, Manchester City kwa kuwa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, itawekwa kibindoni Pauni 53 milioni. Liverpool yenyewe itavuna Pauni 51 milioni, wakati Arsenal inavuna Pauni 46 milioni na Aston Villa, ambayo ni timu ya mwisho kwenye uwakilishi wa Ligi Kuu England katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, itavuna Pauni 33 milioni.

Kwenye Europa League, Tottenham Hotspur iliyomaliza nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu England na kukata tiketi hiyo, yenyewe itaweka kibindoni Pauni 12 milioni kabla hata haijagusa mpira, sawa na kiwango ambacho itavuna Manchester United kwenye michuano hiyo, baada ya kufuzu kwa kupitia tiketi ya ubingwa wa Kombe la FA. Chelsea, yenyewe ambayo ilipokwa tiketi ya Europa League na Man United na hivyo kuhamia kwenye mikikimikiki ya Europa Conference League, itavuna Pauni 5 milioni.

MKWANJA AMBAO TIMU ZA ENGLAND ZITAVUNA KABLA YA KUCHEZA MECHI YOYOTE ULAYA MSIMU HUU

-Man City - Pauni 53 milioni

-Liverpool - Pauni 51 milioni

-Arsenal - Pauni 46 milioni

-Aston Villa - Pauni 33 milioni

-Tottenham - Pauni 12 milioni

-Man United - Pauni 12 milioni

-Chelsea - Pauni 5 milioni

Chanzo: Mwanaspoti