Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila la kheri timu zetu kimataifa

Vigogo Ooo Kila la kheri timu zetu kimataifa

Fri, 16 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kuanzia leo Ijumaa hadi Jumapili, timu zetu tano zinazoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya klabu Afrika zitakuwa uwanjani kuanza kupeperusha bendera katika mashindano hayo.

Jumamosi, Yanga itakuwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuumana na Vital’O ya Burundi, mchezo ambao wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika watakuwa wakihesabika wapo ugenini.

Jioni yake saa 12 jioni, Coastal Union itakuwa ugenini huko Angola ikiumana na Onze Bravos ya huko kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Jumapili, Azam FC itakuwa nyumbani kucheza na APR ya Rwanda katika mechi ya mwanzo ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itaanza saa 12:00 jioni.

Siku hiyo hiyo, timu mbili za Zanzibar nazo zitakuwa uwanjani kucheza mechi zao za nyumbani kwenye mashindano hayo lakini zitakuwa nje ya ardhi ya Tanzania ambazo ni JKU itakayocheza na Pyramids ya Misri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Uhamiaji itakuwa huko Libya kucheza na Al Ahli Tripoli katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Tunaziombea heri timu hizo tano ziweze kufanya vizuri ili ziitoe kimasomaso Tanzania na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua inayofuata ya mashindano ambayo kila moja inashiriki.

Hapana shaka zimefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi hizo na wachezaji watapambana vilivyo kuhakikisha Watanzania wanapata furaha kutokana na matokeo mazuri ambayo zitayapata.

Zicheze zikifahamu mashindano hayo ni magumu na hayatabiriki hivyo zisijiamini kupitiliza ai kudharau timu ambazo zitakutana nazo na nyingine hazitakiwi kuogopa.

Chanzo: Mwanaspoti