Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kila la kheri Taifa Stars

Taifa Stars DUWA 1140x640 Kila la kheri Taifa Stars

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesho Ijumaa, Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ina kibarua cha kucheza dhidi ya Uganda, mechi ya kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (AFCON).

Mchezo huo utachezwa nchini Misri, kisha marudiano kwa timu hizo ni Uwanja wa Mkapa, Dar, Machi 28, mwaka huu.

Wakiwa tayari Taifa Stars wamecheza mechi mbili na kukusanya alama moja katika Kundi F, zimebaki mechi nne za kuisaka nafasi ya kushiriki AFCON nchini Ivory Coast, michuano ikitarajiwa kufanyika mwaka 2024.

Tayari hamasa zimeanza kutolewa kuona Taifa Stars inafanya vizuri na kufuzu AFCON kwani Serikali kupitia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema kuna kitita cha shilingi milioni 500 endapo timu hiyo itafuzu AFCON.

Ni jambo zuri kuona hamasa zinatolewa ili kuwafanya wachezaji kujituma zaidi ndani ya uwanja kwa lengo la kuipa heshima nchi, hivyo kuna deni kubwa kwa wachezaji juu ya Watanzania.

Hata kama bila ya kuwepo kwa hamasa, wachezaji wanapaswa kujituma kwani wamechaguliwa wao kati ya wachezaji wengi kuliwakilisha taifa, hivyo kazi kwao.

Hizi hamasa zinatolewa, ni sehemu tu ya kuongeza nguvu, hivyo wachezaji msiichezee fursa hii ili kuona Tanzania inashiriki tena AFCON baada ya kucheza mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 kule Misri.

Kila la kheri Taifa Stars katika safari ya kufuzu AFCON, Watanzania tupo nyuma yenu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live