Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikosi cha Simba kilichokwea pipa kwenda Uturuki

Simba Uturuki Ers Kikosi cha Simba kilichokwea pipa kwenda Uturuki

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Simba kimeanza safari leo Julai 11, 2023 kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na msimu mpya ujao 2023/24.

Baada ya ratiba ya mechi za Ngao ya Jamii kutoka, Simba itakuwa na takribani wiki tatu za maandalizi kabla ya kuivaa Singida Fountain Gate FC katika mchezo wa Nusu Fainali ambao utapigwa Agosti 10 katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya hiyo, Ahmed Ally amesema kuwa bado hawajamaliza utambulisho, kuna wachezaji wengine wanasubiri kutambulishwa.



“Tunaondoka leo kwenda Uturuki kambini, wachezaji wetu wote watakwenda kushiriki kambi hiyo ya maandalizi. Kocha Robertinho na benchi lake la ufundi wote wako hapa tayari kwa safari”

“Wachezaji wanne wapya tuliowatambulisha nao watajumuika katika kikosi chetu kinachokwenda Uturuki. Bado hatujamaliza, kuna vyuma vingine viwili tutavitambulisha,” amesema Ahmed



Ikiwa Uturuki Simba inatatajiwa kucheza mechi tatu za Kimataifa za kirafiki.

Kikosi Cha Simba kiilichosafiri kwenda nchini Uturuki kwaajili ya pre-season ni;

MAKIPA

Ally Salim

Ahmed Feruzi

MABEKI

Shomari Kapombe

Mohamed Hussein

Henock Inonga

David Kameta

Israel Mwenda

Kennedy Juma

Jimson Mwanuke

Che Fondoh Malone Junior

VIUNGO

Claoutas Chma

Sadio Kanoute

Mzamiru Yassin

Nassoro Kapama

Aubin Kramo Kouamé

Saido Ntibanzonkinza

Peter Banda

Pape Osmane Sakho

WASHAMBULIAJI

Willy Essomba Onana

Baleke Othos Baleke

John Raphael Bocco

Moses Phiri

Kibu Denis

Mohamed Mussa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live