Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijili ataja kinachombeba SBS

Kelvin Kijili Kijili ataja kinachombeba SBS

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki Kelvin Kijili anayecheza katika kikosi cha Singida Big Stars (SBS) ameweka wazi kwamba sababu kubwa inayomfanya awe kwenye kiwango cha juu ni kutokana na ushindani wa namba uliopo baina yake na wenzake.

Kijili amejiunga na Singida BS msimu huu baada akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na kikosi cha KMC.

Kijili alisema kuna changamoto kubwa ya namba kwa sababu wachezaji wote ni wazuri wanaocheza nafasi yake hivyo inamuhamasisha kujituma zaidi.

"Najisikia vizuri sana kuwa kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu ushindani ambao upo ni mkubwa sana, juhudi zangu ni kutokana na ushindani wa hapa;

"Nafanya sana mazoezi, binafsi na timu, pamoja na kujitunza hiyo ndio siri kubwa ya kiwango changu mimi kuhakikisha nakuwa bora,"

Kijiri katika nafasi yake anachuana na wachezaji kutoka nje ya nchi, Nico Wadada (Uganda) na Nicolas Gyan (Ghana) lakini wote wanasubili dhidi yake.

Beki huyo amekuwa na kiwango kizuri tangu msimu uliopita akiwa na KMC hali ambayo imewafanya mabosi wa Singida BS wamsajili msimu huu.

Chanzo: Mwanaspoti