Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiiza atuma salamu Geita Gold

Kiiza Pic Data Hamis Kiiza ‘Diego’

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Hamis Kiiza 'Diego' amesema kilio cha benchi la ufundi cha mastarika wa timu hiyo kukosa mabao wamekisikia na kesho wanakwenda kuonyesha tofauti dhidi ya Geita Gold kwa kufunga na kulinda ushindi ili kutoendelea kugawa pointi kwa matajiri hao wa Dhahabi.

Kagera Sugar imeanza ligi kwa vichapo mfululizo ikifungwa 2-1 na Azam na 2-0 dhidi ya Simba ambapo kesho itashuka katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa kuivaa Geita Gold katika mchezo wa raundi ya tatu Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Kiiza amesema changamoto zote zilizojitokeza katika michezo hiyo zimefanyiwa kazi kwenye mechi mbili za kirafiki jijini hapa wakifunga mabao 10 hivyo safu ya ushambuliaji inaahidi neema kesho.

"Washambuliaji tutajitahidi kutafuta mabao na isiishie hapo bali kuisaidia pia timu kulinda ushindi kwa sababu mchezo wa Azam tulitangulia lakini tukashindwa kulinda bao letu. Kesho tunakwenda kupambana ili tusipoteze tena pointi zingine mbele ya Geita Gold,"

"Tunakwenda kupambana kuona tunaanza vizuri sisi wenyewe tumeona nafasi tuliyopo tunajua hatustahili kuwa pale, tunajua umuhimu wa mchezo huu na wachezaji tumezungumza kuhakikisha tunafanya vizuri," amesema Kiiza.

Akizungumza kwa niaba ya benchi la ufundi, Kocha wa Makipa wa timu hiyo, John Wawa, amesema hawatakubali kwa mara nyingine kufungwa na Geita Gold kwani kila kitu kinachotakiwa kupata ushindi wamekifanyia kazi na wana imani kubwa ya kuibuka na ushindi kesho.

"Tumejiandaa vyema baada ya kilichotokea katika michezo miwili ya nyuma tunaamini tutakuja na ushindi kesho dhidi ya Geita,"

"Mapumziko ya wiki mbili yametupa nguvu ya kujiandaa vizuri na kufanyia kazi makosa machache yaliyotugharimu michezo iliyopita, tunakwenda kuonyesha tofauti na msimu uliopita ambao tulipoteza pointi sita kwao," amesema Wawa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live