Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiingilio Stars 2000

69691 Pic+stars

Sun, 4 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KATIKA kile kinachoonekana mbinu ya kuongeza hamasa kwa mashabiki wao kwenye mechi dhidi ya Taifa Stars, Shirikisho la Soka Kenya (FKF) limetangaza kushusha bei ya kiingilio kwa mashabiki wa soka nchini hapahadi Sh 2000 ya Kitanzania

Mechi hiyo ni ya marudiano ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (Chan).

Rais wa FKF, Nick Mwenda amesema lengo la kuweka bei ya chini ya kiingilio ni kuvuta umati wa mashabiki watakaoipa sapoti timu yao ya taifa.

"Sio kama Wakenya hawapendi mpira. Wanapenda na ndio maana walikuja kwa idadi kubwa kwenye mechi dhidi ya Ghana, Ethiopia na hata Everton walipokuja hapa.

"Jambo la msingi la kuwavuta mashabiki ni kupata matokeo mazuri. Na pamoja na hilo pia tumeweka kiingilio kwa bei ya Shilingi za Kenya 100 (Sh 2,260 ya Tanzania) ili waje zaidi. Kikubwa tunaiheshimu Tanzania lakini tuna uhakika wa kupata ushindi," amesema Mwenda.

Chanzo: mwananchi.co.tz