Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kihinga kuongeza ushindani wa Yanga kimataifa

Yanga Shirikishoz Kihinga kuongeza ushindani wa Yanga kimataifa

Wed, 6 Jul 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mgombea ujumbe wa kamati ya utendaji Yanga, Gerald Kihinga amesema kitu kilichomvutia kujitosa kugombea nafasi hiyo ni kuunga mkono juhudi za kuifanya klabu hiyo iwe na ushindani kimataifa.

Amesema kutokana na kuipenda Yanga alikuwa anawaza siku moja atakuja kuifanyia makubwa, baada ya kuona mgombea Urais injinia Said Hersi ameweka vipaumbele vyake akaona ni wakati sahihi wa kuungana naye.

"Nimeamua kugombea nafasi ya ujumbe kamati ya utendaji Yanga kwa sababu ni klabu ninayoipenda, kilichonivutia zaidi niĀ  vipaumbele vya mgombea Urais injinia Hersi ambaye anataka kuleta mabadiliko makubwa katika soka la Tanzania,"amesema na ameongeza;

"Jambo lingine ni kuhakikisha tunajenga Uwanja wa Kaunda, ambao utawafanya Wanayanga kufika kirahisi kuishuhudia timu yao ikicheza, hivyo vyote vitatimia tukiunganisha maarifa yetu kwa pamoja ." Mbali na hilo, akifanikiwa kuchaguliwa anaamini atakuwa na mchango wa namna Yanga inaweza ikanyakua taji la ubingwa wa Afrika.

"Kama nitachaguliwa kwa kushirikiana na rais ajaye, basi tunataka Yanga iwe ya kwanza kulileta taji la Afrika nchini, hilo linawezekana kwani, itatokana na kuwa na vitega uchumi imara vitakavyotuwezesha kusajili wachezaji wa viwango vya juu,"amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz