Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigwangalla: Mangungu hana tatizo, Simba mtoeni Mo Dewji

Kigwangallah A.png Dk. Hamisi Kigwangalla.

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Nzega Vijijini na shabiki wa Klabu ya Simba, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla amewashauri mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kumuondoa mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji akidai kuwa ndiyo chanzo cha matatizo yote ndani ya klabu hiyo.

Kigwangalla amesema hayo baada ya Simba kufungwa bao 5-1 na watani zao Yanga huku mashabiki wakishinikiza Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Abdallah Salim 'try Again' wajiuzulu.

Kupitia ukurasa wa twitter, Kigwangallh amesema; "Kwa nini Wadau mnaibua haya baada ya kukandwa khamsa na watani zetu? Wakati ule nasema kuhusu shida za mifumo ya utawala na fedha ndani ya Simba SC, kila mtu alifurahia spinning ya mwekezaji wetu kuwa nina chuki sababu alininyima mkopo wa pikipiki! Hoja yangu ya msingi ilipuuzwa. Nendeni mkatazame nilikuwa nahoji nini? Mtagundua mlivyo nyuma ya wakati!

"Ndugu yangu Mangungu hana shida namfahamu vizuri, uwezo wake wa uongozi, ufuatiliaji na ubunifu ni mkubwa mno usio na shaka! Kama mnataka kuzungumzia mfumo/muundo wa governance ya Simba, izungumzeni yote kwa utimilifu wake! Kwa sasa mtuache tuuguze majeraha yetu. Kupigwa khamsa siyo jambo la ajabu! Ndiyo mchezo ulivyo. Hata sisi tuna rekodi ya kuwapiga Uto 6, Mara 5!

"Kwa uchache tunapaswa kufanya haya: 1.) weka mfumo/Muundo mzuri wa utawala 2.) weka Mfumo wa kusimamia raslimali fedha na raslimali watu 3.) weka standard operating procedures/rules kwenye kuajiri na kusajili/kuachana na wachezaji na waalimu 4.) weka codes zitakazoongoza aina na namna ya mikataba ya raslimali watu 5.) weka sera za fedha, sera za raslimali watu zinazojulikana 6.) ajiri professionals kusimamia hii mifumo/miundo uliyoweka!

"Achaneni na Mangungu, toeni mwekezaji janja janja kama nyie wanaume kweli! Na kama mnajua tatizo linapoanzia! Halafu wanataka kuhangaika na Mangungu wa watu ambaye amevishwa koti la Mwenyekiti huku hasikilizwi, anapuuzwa, mamlaka yake ya kikatiba yanapuuzwa, na wala klabu haifuati taratibu zozote zile za ki-corporate!

"Niseme nisiseme? Acha niseme tu! Mangungu, Try Again na wengine hawana shida kabisa…Glazer ni tapeli, janja janja, fitna na bahili kweli kweli! Siyo kama Ghalib ama Yusuf, wale wamenyooka, wanatupia mzigo wa Maana kwenye timu! Sisi mpaka leo Glazer hajalipia hisa zake.

"I repeat mpaka leo hii! Ni miaka mingapi hiyo? Unajua sababu yake? Ulidhani GSM tungemjua bila Manji kuondoka Yanga? Ukitaka kwenda peponi lazima ufe kwanza," amesema Kigwangallah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live