Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigonya apewa mkono wa kwaheri Azam FC

Kigonya Pic Mathias Kigonya

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Uongozi wa Azam FC umefikia makubaliano ya pande mbili kwa ajili ya kuvunja mkataba na aliyekuwa kipa wake Mganda, Mathias Kigonya.

Mara baada ya msimu wa 2021/22 kumalizika nyota huyo alibakiza miezi sita kwenye mkataba wake huku akiwaomba viongozi wa kikosi hicho kuomba kuondoka ili akapate changamoto sehemu nyingine msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa na timu hiyo ilieleza kumshukuru Kigonya katika kipindi chote alichoitumikia tangu alipoajiunga nayo Januari mwaka jana akitokea Forest Rangers ya Zambia.

Huyo ni nyota wa pili kuachwa na Matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam msimu huu baada ya hapo awali kuachana na kiungo wake Frank Domayo 'Chumvi'.

Chanzo: Mwanaspoti