Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigoma full Shangwe ujio wa Yanga

Yanga 4 Kikosi cha Yanga

Mon, 18 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ruvu Shooting wenyeji wa pambano la Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, wameamua kulipeleka pambano hilo mkoani Kigoma, jambo lililowapa furaha wenyeji wa mkoa huo na kuwashukuru Wazee wa Kupapasa kwa walichokifanya.

Uongozi wa Ruvu umetumia kanuni ya 9(7) inayoruhusu klabu kuhamisha mechi zao mbili za nyumbani kwenye viwanja visivyokuwa na mechi za Ligi Kuu na sasa mchezo wao wa Mei 4 dhidi ya Yanga utapigwa Uwanja wa Lake Tanganyika.

Kitendo hicho kimemfanya Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Kigoma (KFA), Omary Gindi kufunguka na kudai hiyo kwao imekuwa fursa na kuishuruku Ruvu kwa uamuzi wao huo.

Akizungumza Gindi alisema uwepo wa Yanga kwenye mkoa huo ni fursa nyingine kwa wafanyabiashara kutokana na uwepo wa mashabiki wengi.

“Yanga ni timu kubwa na popote pale inapocheza inatoa fursa kubwa kwa wakazi wa maeneo husika, hivyo kwa kweli tunawashukuru viongozi wa Ruvu Shooting kwa kutuletea mchezo huu hapa mkoani kwetu,” alisema Gindi na kuongeza;

“Sio watu wote wenye uwezo wa kuzishuhudia hizi timu kubwa za Simba, Yanga kule Dar es Salaam ila zinapotoka na kuja huku hakika zinaamsha motisha ya timu zilizopo chini kupambana na wao kupata nafasi hii.”

Mara ya mwisho kwa Yanga kucheza kwenye uwanja huo ilikuwa Julai 25, mwaka jana ilipofungwa bao 1-0 na Simba katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Katika mchezo wao wa kwanza msimu huu dhidi ya Ruvu, Yanga ilishinda mabao 3-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live