Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo Yanga azipa nafasi Simba na Yanga kutoboa nusu fainali

Simba X Yanga CAF Kigogo Yanga azipa nafasi Simba na Yanga kutoboa nusu fainali

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Yanga SC , Arafat Haji kupitia uharasa wake wa Twitter amezipa nafasi ya kufuzu kwenda nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika timu za Simba na Yanga.

Katika andiko lake Arafat amesema "Kuhusu nafasi ya Yanga kuvuka hatua ya robo fainali, nafasi kwanza ipo kubwa kwa wote wawili kufika nusu fainali ila kwasasa inahitajika MIPANGO YA MUDA MFUPI ndani ya Mipango ya muda mrefu.

Nyuma ya RS Berkane kutwaa shiirkisho, USMA kubeba Shirkisho kulikuwa na plans zinazobadilika kulingana na hatua, natolea mfano timu ambazo hazikuwahi kupewa nafasi kubwa Afrika ila wamefanya vyema hivi karibuni"

Mwisho anasema "Ukitazama kwa haraka ni support ya serikali na Wadau, inapokuja suala la klabu zao kimataifa wote wanaimba wimbo mmoja kwa maslahi ya kiwanda chao, sehemu ya kwanza ni UMOJA".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live