Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo Yanga atamba baada ya kumbakisha Mayele

Mayele, Lomalisa Moloko Fiston Mayele

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga, umeweka wazi mpango wake wa kushusha vifaa vya maana kwa ajili ya kuhakikisha msimu ujao timu inaendelea kufanya vema ikiwemo kuwabakiza mastaa wake ambao bado wana umuhimu mkubwa kwa timu akiwemo Fiston Mayele.

Hiyo ikiwa ni siku chache baada ya kumtangaza Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi ambaye amekuja kurithi mikoba ya Nasreddine Nabi.

Yanga mpaka sasa bado haijatangaza usajili wa mchezaji wapya, huku tayari wakiwaacha baadhi ya mastaa wao kama Tuisila Kisinda, Bernard Morrison, Dickson Ambundo na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Wakati ikiachana na nyota hao, inapambana kumbakisha Fiston Mayele ambaye kutokana na uwezo mkubwa aliouonesha msimu wa 2022/23, klabu tofauti zimeanza kumuwinda zikiwemo kutoka Afrika Kusini na Uarabuni.

Akizungumza nasi, Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji, alisema kuwa uongozi tayari unafanya kazi kwa ajili ya kuhakikisha unafanya kile liwezekanalo ili kuifanya timu kuendelea kuwa tishio msimu ujao.

“Yanga kama viongozi tumefanya kazi nzuri msimu uliopita na tunafurahi kuona timu imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, hivyo ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuhakikisa msimu ujao tunayafikia mafanikio ambayo tuliyafikia msimu uliopita.

“Kikubwa tunachotaka kukifanya ni kuhakikisha tunafanya usajili wa maana ambao utaongeza nguvu kwenye kikosi chetu, lakini pia kuwabakisha wale wote ambao ni muhimu kwa timu, watu wanatakiwa kuwa watulivu na watashuhudia vyuma vya maana vikitua Yanga katika dirisha hili linalokuja la usajili,” alisema kiongozi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: