Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo TFF: Azam wanaongea siasa tu, huenda hizo milioni 700 hazimo kwenye mkataba

Mvela Dube Kigogo TFF: Hakuna aliyeuona mkataba wa Prince Dube

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria na Wananchama wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Eliud Mvela, amesema kuwa, hakuna anayeufahamu mkataba wa mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube na klabu yake hiyo.

Mvela amesema kuwa huenda hata hizo Tsh milioni 700 wanazotaka Azam walipwe na Dube au klabu inayomtaka ili kuvunja mkataba, hazijaandikwa kwenye kipengele chochote cha mkataba jambo ambalo amesema kuwa ni siasa za mpira tu.

“Hakuna aliyeuona Mkataba wa Azam na Dube na kama Dube angeona mkataba ni wa thamani kubwa kuvunjwa asingeingia katika vita hii. Na kule anakotaka kwenda wameona mashariti ya mkataba yapo ndani ya uwezo wao.

“Inawezekana kauli za Tsh milioni 700 Azam wanaongea siasa tu lakini si ajabu hizo milioni 700 hazimo katika mkataba. Timu za Bongo mwisho wataishia kukaa chini na kumalizana kama ilivyokuwa kwa Feisal,” amesema Mvella.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live