Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo Simba amkataa Robertiho, amuita shabiki tu

Azim Dewji Kauli Aliyekuwa mfadhili wa klabu ya Simba, Azim Dewji

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wingu zito likizidi kutanda kunako klabu ya Simba SC ikianziwa na hatima yao kunako michezo ya hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bado Ubingwa wa Ligi Kuu nao pengo kati yao na vinara Yanga linazidi kuwa kubwa baada ya sare yao na Azam FC juzi na sasa ikiwa ni alama 8.

Kwa matukio hayo mawili makubwa tayari hali ya hewa ndani ya Simba inaonekana kutokuwa shwari kwani wapo mashabiki wanaotaka uongozi ung'oke, lakini kuna wale wanaomnyooshea kidole Kocha Robertinho.

Sasa kubwa kuliko yote ni kauli ya Aliyekuwa mfadhili wa klabu ya Simba, Azim Dewji amesema anamtambua Juma Mgunda kama kocha Mkuu wa klabu hiyo na sio Robertinho.

"Binafsi namtambua Juma Mgunda kama kocha mkuu wa klabu ya Simba, Robertinho ni kama shabiki tu".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live