Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo PSG amchana vibaya Kylian Mbappe

Kylian Mbappe 1.jpeg Kigogo PSG amchana Kylian Mbappe

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuugenzi wa Michezo wa zamani wa PSG, Leonardo amemtaka nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe kuondoka Klabuni hapo na kwenda mahali anapopataka.

Leornado ambae alikuwa sehemu kubwa ya kumshawishi mbappe kusaini Mkataba wa miaka miwili na nyogeza ya mwaka mmoja Disemba 2022 kabla ya kuondolewa katika nafasi yake mwishoni mwa msimu wa mwaka 2021/22.

Akizungumza katika moja ya mahojiano Leornado amesema;

"Kwa faida ya Klabu, ni wakati wa Mbappe kuondoka haijalishi yeye ni nani"

"PSG ilikuwepo kabla ya Mbappe na itaendelea kuwepo bila Mbappe . Yupo Paris kwa miaka sita, na katika hiyo miaka sita kuna timu tano tofauti zimetwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya ."

Mkataba wa Mbappe unaisha Juni 2024, na tayari PSG wametangaza kumweka sokoni ikiwa hatotaka kuongeza Mkataba huku Real Madrid wakiongoza mbio za kumfukuzia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live