Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo Napoli atoa neno usajili wa Victor Osimhen

Victor Osimhen Hauzwi.jpeg Victor Osimhen

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio de Laurentiis amesema hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji wao matata ndani ya klabu hiyo Victor Osimhen.

Mshambuliaji Victor Osimhen amekua akifuatiliwa na vilabu kadhaa kutoka ligi kuu ya England kama Manchester United,Chelsea,na klabu ya Liverpool pia ikitajwa, Lakini rais wa klabu ya Napoli yeye amesisitiza hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria mpaka sasa anaongoza kw mabao katika ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A huku akifanikiwa kuifanya klabu yake ya Napoli kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo mpaka sasa.

Victor Osimhen amekua kwenye kiwango bora sana msimu huu tangu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2020 akiwa amehusika kwenye mabao 20 mpaka sasa, Huku akiwa amefunga mabao 17 na kupiga pasi tatu za mabao na kufanya idadi kufika 20.

Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis amesisitiza kua wachezaji wao ni muhimu zaidi kwenye timu hiyo hivo hawalazimishwi kuwauza wachezaji wao, Hii inaonesha wazi kua rais huyo hana mpango wa kumuachia Osimhen pamoja na mchezaji wake yeyote muhimu kikosini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live