Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo Man United azuia dili la Todibo

Gatdygxf Kigogo Man United azuia dili la Todibo

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mazungumzo baina ya Manchester United na Nice juu ya usajili wa Jean Clair Todibo yalifikia patamu lakini kwa sasa yamesitishwa kutokana na sheria za Uefa kwa sababu mmiliki wa Nice, Jim Ratcliffe pia ana hisa ndani ya Man United.

Todibo mwenye umri wa miaka 24, alikuwa akihitajika na Man United baada ya kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita akiwa na Nice ambayo imefuzu kucheza Europa League.

Man United ilimhitaji Todibo kama sehemu ya mpango wao wa muda mrefu wa kujenga kikosi kitakachowapa mafanikio kwa miaka mingi kutokana na umri.

Kushindikana kwa dili hili kunafungua milango zaidi kwa beki wa Everton, Jarrad Branthwaite kujiunga na mashetani hawa wekundu.

Hata hivyo, Man United imekuwa ikisuasua katika dili la Branthwaite kutokana na kiasi kikubwa cha pesa ambacho Everton inakihitaji kuwa ni kikubwa tofauti na bajeti yao.

MANCHESTER United bado inapambana kuhakikisha inaipata saini ya straika wa Lille na Canada, Jonathan David, 24, dirisha hili kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji. Katika msimu uliopita staa huyu alicheza mechi 47 za michuano yote na kufunga mabao 26. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2025.

LICHA ya vigogo wengi barani Ulaya ikiwemo Bayern Munich na Inter Milan kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Manchester United na Ureno, Bruno Fernandes dirisha hili, mabosi wa mashetani hao wekundu inadaiwa hawajaweka suala la kumwongeza mkataba mpya staa huyo katika dirisha hili. Mkataba wa sasa wa Bruno unamalizika mwaka 2025.

KIUNGO wa Fiorentina na Morocco, Sofyan Amrabat, 27, amewaambia mabosi wa timu yake hahitaji kurudi tena msimu ujao na badala yake anataka kutua timu nyingine kubwa ama kuendelea kusalia Manchester United aliyoichezea kwa mkopo msimu uliopita.

Amrabat alicheza mechi 30 za michuano yote msimu uliopita alipokuwa na Man United. Mkataba wake na Fiorentina unamalizika mwaka 2025.

BAYERN Munich imemweka katika nafasi za juu katika orodha ya wachezaji inaohitaji kuwasajili dirisha hili, kiungo wa Paris St-Germain, Xavi Simons, 21. Hata hivyo, inapambana kuishawishi PSG ikubali kumuuza staa huyu wa kimataifa wa Uholanzi kwa bei ya chini tofauti na ile ya sasa ya Pauni 84.4 milioni.

WEST Ham inapata wakati mgumu katika kumbakisha winga wao raia wa Ghana, Mohammed Kudus, katika dirisha hili kutokana na kuwepo kwa matajiri wa Al Ittihad kutoka Saudi Arabia ambao wapo tayari kumpa mshahara wa zaidi ya Pauni 300,000 kwa wiki ili kuipata saini yake. Mkataba wa winga huyu mwenye umri wa miaka 23, unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

LEICESTER City na Fulham zimeripotiwa kuwa katika hatua nzuri kwenye mchakato wa kuiwania saini ya kiungo wa AS Roma, Edoardo Bove dirisha hili ingawa timu nyingine za England Everton na Bournemouth pia zinajaribu kupambana kuhakikisha zinaipata huduma yake. Kiungo huyu raia wa Italia, mkataba wake unamalizika mwaka 2028. Msimu uliomalizika alicheza mechi 45 za michuano yote.

FULHAM inataka kumpa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja kiungo wao raia wa Brazil, Willian, 35, ambaye ameonyesha kiwango bora msimu uliopita. Licha ya ofa hiyo ambayo Fulham inaiandaa, kuna ripoti baadhi ya timu za Saudi Arabia zinataka kumsajili staa huyu. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa mwezi huu.

Chanzo: Mwanaspoti