Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo Barcelona apitisha jina la Luis Diaz

LUIS Diaz Ff Luis Diaz

Mon, 27 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco ni shabiki mkubwa wa winga wa Liverpool, Luis Diaz na huenda akatoa ruhusa ya kuuzwa kwa Raphinha ili pesa zitakopatikana zitumike kumsajili staa huyo wa kimataifa wa Colombia.

Baba mzazi wa staa huyu ameshawahi kusema mara kadhaa mwanawe ana ndoto ya kucheza Hispania kati ya moja ya timu kubwa Real Madrid au Barcelona.

Hata hivyo, Diaz ameonyesha kiwango bora kwa msimu uliopita na alicheza mechi 51 za michuano yote na kufunga mabao 13.

Diaz mwenye umri wa miaka 27, mkataba wake na Liverpool unamalizika mwaka 2027.

Taarifa za kuondoka kwake zimezidi kuchochewa katiuka miezi ya hivi karibuni tangu alyekuwa kocha wao Jurgen Klopp kutangaza kwamba hatoendelea kuifundisha timu hii.

KIUNGO wa Manchester City na Ubelgiji, Kevin de Bruyne amepanga kuendelea kusalia katika timu hiyo ikiwa dili lake la kwenda Saudi Arabia litafeli katika dirisha lijalo. Wawakilishi wa fundi huyu tayari wameshatua Saudi Arabia kwa ajili ya kuzungumza na baadhi ya timu. Awali ilielezwa de Bruyne mwenye umri wa miaka 32, anaweza akaondoka mwisho wa msimu hata kama sio Saudi Arabia.

MSHAMBULIAJI wa West Ham, Jarrod Bowen anataka kuendelea kusalia kikosi hicho kwa msimu ujao licha ya timu mbalimbali kama Newcastle United kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. Bowen mwenye umri wa miaka 27, mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2030. Msimu uliomalizika amecheza mechi 44 za michuano yote, amefunga mabao 20 na kutoa asisti 10.

WAWAKILISHI wa kiungo wa Arsenal, Emile Smith Rowe wanatarajiwa kuingia katika mazungumzo na mabosi wa timu hiyo kuanzia wiki ijayo ili kujadili hatma ya staa wao baada ya msimu uliomalizika kutopata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Inaelezwa anataka kuondoka kutafuta timu nyingine itakayompa nafasi kubwa ya kucheza tofauti na ilivyo sasa.

BARCELONA imeshawasiliana na kiungo wa Liverpool, Thiago Alcantara ambaye anaondoka timu hiyo mwisho wa msimu huu ili wamsajili aende kuwa mchezaji lakini pia msaidizi wa kocha mpya Hansi Flick. Ifikapo Juni 30, Alcantara mkataba wake utakuwa umemalizika na Liverpool haionekani kuwa na mpango wa kutaka kumuongeza.

PARIS St-Germain imetuma ofa ya Euro 100 milioni kwenda Napoli kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Khvicha Kvaratskhelia, katika dirisha lijalo. Kumekuwa na timu nyingi zinazotajwa zinahitaji kumsajili Khvicha tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, lakini changamoto imekuwa kwa Napoli ambayo haijaonyewsha nia ya kumuuza hado sasa.

PSG ina matumaini madogo ya kuipata huduma ya beki wa kati wa Lille, Leny Yoro baada ya Liverpool, Manchester United na Real Madrid kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. Mchezaji huyu amebakisha msimu mmoja katika mkataba wake na Lille ambayo ipo tayari kumuuza kwa ofa nzuri kwani wakikaa naye kwa msimu ujao anaweza akaondoka kwa pesa ndogo Januari.

ASTON Villa imeweka wazi inahitaji walau Pauni 6 hadi 8 milioni kwa ajili ya kumuuza kiungo wao kutika Brazil Philippe Coutinho, 31, dirisha lijalo ingawa ipo tayari kumtoa kwa mkopo kwa timu itakayohitaji kumchukua. Coutinho amekuwa na wakati mgumu tangu atue Villa na alitolewa kwa mkopo kwenda Qatar na sasa ripoti zinadai anataka kurudi Brazil.

Chanzo: Mwanaspoti