Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo Barca awakataa, Klopp, Arteta na PEP

Bosi Wa Zamani Wa Arsenal Adai Arteta 'amechafua Picha Ya Klabu' Kigogo Barca awakataa, Klopp, Arteta na PEP

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati tetesi juu ya kocha mpya anayeweza kuchukua mikoba ya Xavi Hernandez pale Barcelona zikiendelea, mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Deco, ameweka wazi kwamba Jurgen Klopp, Pep Guardiola na Mikel Arteta hawawezi kuwa makocha wa timu hiyo.

Barca imeingia kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya baada ya Xavi kutangaza ataondoka mwisho wa msimu baada ya kudumu kwa misimu mitatu.

Kocha wa kwanza aliyehusishwa kuwa kwenye rada zao ni kocha wa Arsenal, Arteta akifuatiwa na kocha wa City, Guardiola na Klopp wa Liverpool. Lakini Deco amesema haiwezekani.

“Kweli kabisa inabidi uheshimu makocha wakubwa kama Guardiola, Klopp na Arteta lakini hawapatikani, hakuna mazungumzo yanayoendelea baina yetu na wao, ni kupoteza muda tu kusema tunawataka, ukweli ni kwamba hatupo kwenye mazungumzo na kocha yeyote kati yao.”

Iliwahi kuripotiwa mwanzoni mwa Machi kwamba wababe hawa kutoka Camp Nou wameshaanza mazungumzo na Arteta kwa ajili ya kujiunga nao mwisho wa msimu huu.

Mbali ya Arteta ikaelezwa kocha wa Brighton, Roberto De Zerbi naye amewekwa kama mbadala ikiwa mchakato wa kumchukua mwalimu huyo wa washika mitutu wa Jiji la London utafeli.

Ukiondoa makocha hawa ambao Deco amesema hawapo kwenye mazungumzo nao, kuna tetesi zinazomhusisha Hansi Flick na Thomas Tuchel kwamba wanaweza kuajiriwa huku Flick akipewa nafasi kubwa zaidi kwa sababu ana ukaribu na rais wa timu hiyo Joan Laporta.

Chanzo: Mwanaspoti