Kifo cha wakala mkubwa duniani Mino Raiola ni pigo kubwa kwenye tasnia ya mchezo wa mpira wa miguu wamepata huku akiacha simtofahamu kubwa kwenye soko la uhamisho wa wachezaji ambao alikuwa akiwasimamia.
Wakala huyo kutoka Italia Mino Raiola kazi zake za uwakala zimeamishiwa kwa ndugu yake Vincenzo, ambaye atakuwa na kazi ngumu ya kuendeleza kazi zake, na kufanya wateja wa Riola kuwa na furaha na ni muda wake ya kuonesha uwezo wake sasa baada ya kufanya kazi na ndugu yake kwa muda mrefu.
Baadhi ya mawakala wakubwa sasa wanajiandaa kuchukua wateja wa Mino Raiola, ambao ni Jonathan Barnett, Jorge Mendes, Volker Struth, Pini Zahavi na Alessandro Lucci. Enzo Raiola sasa ana kazi kubwa ya kufanya kuweza kuwabakisha wateja wa ndugu yake na kuboresha ubora wa soko lake la usajiri.
Mino Raiola mikataba minono ambayo aliwai kuifanikisha ni:-
Matthijs De Ligt – Juventus – 2024 – €90milion
Erling Haaland – Borussia Dortmund – 2024 – €75milioni
Gianluigi Donnarumma – PSG – 2026 – €65milioni
Marco Verratti – PSG – 2024 – €60milioni
Ryan Gravenberch – Ajax – 2023 – €40milioni
Paul Pogba – Manchester United – 2022 – €40milioni
Hirving Lozano – Napoli – 2024 – €30milioni
Moise Kean – Juventus – 2023 – €30milioni
Donyell Malen – Borussia Dortmund – 2026 – €30milioni