Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kifo cha Ally Sonso chaitesa Ruvu Shooting

Screenshot 20220226 173127 Facebook Kifo cha Ally Sonso chaitesa Ruvu Shooting

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa ‘Master’ amesema msiba wa beki wao, Ally Mtoni ‘Sonso’ bado unawatesa nyota wa kikosi cha timu hiyo na kama kocha ameamua kukomalia kuwajenga kisaikolojia ili wakae sawa.

Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, alisema licha ya ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Tanzania Prisons bado amewaona wachezaji wake hawako vizuri kutokana na kuondokewa na mchezaji mwenzao.

“Itawachukua muda kidogo kurudi katika hali yao ya kawaida ukizingatia hata mchezaji aliyekuwa akilala naye chumba kimoja bado hajawa sawa kisaikolojia, hivyo naendelea kuwajenga li kurejea kwenye hali zao za kawaida,” alisema Mkwasa na kuongeza;

“Tunaendelea na maandalizi ya michezo yetu inayofuata, kama unavyojua hatupo katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi, hivyo tunahitaji kupambana ili tuweze kujinasua kwenye nafasi za chini.”

Sonso aliyewahi kuzichezea Lipuli, Yanga, Kagera Sugar na pia timu ya taifa, Taifa Stars alifariki dunia Februari 11, 2022, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na matatizo ya mguu.

Ruvu kwa sasa ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 15 baada ya kushuka uwanjani katika mechi 15, ikishinda nne, sare tatu na kupoteza nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live