Ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally wamekuwa kivutio katika Uwanja wa Manungu Complex ambako timu zao zinacheza jana.
Kitendo cha wawili hao kusalimiana na kufanya mazungumzo mafupi, kilishangiliwa na mashabiki waliokuwa wamesimama jirani na jukwaa kuu.
Kifaru ambaye timu yake ni mwenyeji, alienda kumpokea Ahmed Ally mara baada ya kushuka kwenye basi na kisha kumsalimia kwa kumkumbatia.
Baada ya kukumbatiana, wawili hao walifanya mazungumzo ya hapa na pale huku kila mmoja akisikika akimpongeza mwenzake kisha Ahmed Ally akapanda kwenda katika viti vya jukwaa kuu.
Idadi kubwa ya mashabiki walionekana kurekodi tukio hilo na wengine kupiga picha kwa kutumia simu zao.