Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kieran Trippier: Natumai nitamnyamazisha Kylian Mbappe

Kieran Trippier: Natumai Nitamnyamazisha Kylian Mbappe Kieran Trippier: Natumai nitamnyamazisha Kylian Mbappe

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Winga wa upande wa kulia wa klabu ya Newcastle Kieran Trippier ana matumaini ya kumnyamazisha mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe wakati timu zao zitakapkutana siku ya Jumatano hata iwapo hatua hiyo itamkasirisha mwanawe mdogo.

PSG inazuru uwanja wa James Park katika mechi ya kimakundi ya ligi ya mabingwa Ulaya, lakini mwanawe Trippier anampenda sana Kylian Mbappe.

‘’Anampenda sana kila mara anatazama vídeo zake katika mtandao wa You Tube’’ , alisema Trippier mwenye umri wa miaka 33.

Beki huyo alitoa mzaha kwamba mwanawe angependelea kutembea na Mbappe badala yake. "Sikufurahishwa na hilo’’ , Tripper aliongeza. ‘’Nilimwambia , iwapo utatembea na Mbape usiniangalie’’.

Newcastle inacheza mechi hiyo katika kundi F ikiwa bado haijafungwa katika mechi tano , ikishinda nne ikiwemo ushindi wa magoli 8-0 dhidi ya Sheffield United.

Chanzo: Bbc