Wakati Simba ikifanikiwa kupenya kwa mbinde hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Power Dynamos.
Wengi wameonekana kulalamika na kutilia shaka kiwango cha Timu hiyo hasa katika hatua za mbele za michuano hiyo mikubwa ya ngazi ya Vialabu Afrika.
Mchambuzi kutoka Clouds FM Amri Kiemba anasema kuwa Simba wana wachezaji lakini hawana timu, katika uchambuzi wake Kiemba anasema;
“Simba inashindwa kucheza ndani ya kiwanja kwa namna ambavyo ilikuwa imezoeleka kama utamaduni na inashindwa kwa sababu sasa hivi haina ID ya uchezaji (utambulisho/style of play)."
“Simba ina wachezaji ndani ya kiwanja lakini timu kama timu hakuna, ndicho ambacho kinaleta utofauti wa Yanga na Simba kwa sasa hivi, kuhusu mpinzani Simba imecheza mechi ngumu zaidi ya hii (Power Dynamos)."