Wakati Simba wakijiandaa kuivaa Vipers leo Machi 7 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba inahitaji alama tatu kwa kila namna ili tu kuweka sawa mazingira ya wao kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali ambayo kwa miaka ya karibuni wamekuwa wakikomea hatua hiyo.
Sasa mchambuzi wa soka na mchezaji wa zaman wa Tanzania, Amri Kiemba ametoa maoni yake kuelekea mchezo huo;
"Kuna Mtu naona kama Simba imempoteza kwa maana haipati tena kile alichokuwa anatoa , Augustine Okrah kwa wakati amejitambulisha pale Simba alikuwa ni miongoni mwa Wachezaji wenye uwajibikaji mkubwa sana na aliongeza kasi eneo la pembeni, ni kama Chikwende ambaye alikuja Simba akiwa na silaha ya kasi lakini baada ya kuingia akakuta visigino , kitu ambacho kikawa hakimpi nafasi"
"Hiko ndicho ambacho nakiona kwa Okrah kimemtokea,hatuoni tena akiwa analazimisha mashambulizi sasa hivi na yeye anapiga visigino , lakini kama atakuja na njia sahihi ambayo alijitambulisha nadhani ni miongoni mwa Watu wanaopaswa kuanza leo"
Simba ipo Kundi C sambamba na timu za Raja Casablanca wenye alama (9), Horoya (4), Simba (3) na Vipers wakiburuza mkia (1).