Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiemba: Nilijua mapema Simba hawezi kubeba ubingwa

Simba Imedumaa, Haipigi Hatua   Amri Kiemba Amri Kiemba

Wed, 1 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia Clouds Media, Amri Kiemba, Mchambuzi amesema kuwa alijua mapema kwamba Klabu ya Simba hawataweza kuchukua ubingwa msimu huu.

Simba mpaka sasa wapo nafasi ya tatu ya Ligi Kuu ya NBC wakiwa na alama 47 nyuma ya Azam (54) na Yanga (62).

"Tangu msimu unaanza mimi ni miongoni mwa watu ambao walikutana na upinzani mkubwa sana kwa sababu nilikuwa siamini kama Simba wanaweza kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kwa sababu ya mabadiliko wanayoendelea kuyafanya kwenye timu yao.

"Nilikuwa naamini kuwa wataweza kutetea nafasi ambayo walimaliza msimu uliopita lakini wakiendelea kuimarika. Simba wao waliendelea kuamini wapo tayari kuchukua ubingwa msimu huu.

"Simba walianza kutuonesha kuwa hawapo tayari kutwaa ubingwa wa Ligi msimu huu tangu kwenye mechi za Ngao ya Jamii. Walifanikiwa kuchukua ubingwa wa Ngao ya Jamii lakini hawakuonesha kiwango kizuri uwanjani.

"Kama ubingwa ungekuwa unatolewa kulingana na kiwango cha timu uwanjani, Simba ingekuwa timu ya mwisho [4]. Yanga wangekuwa namba moja, Azam wangefuata, Singida Fountain Gate halafu Simba wangemaliza.

"Simba kuwa bingwa wa Ngao ya Jamii kulificha mapungufu yao mengi sana na watu wakajificha humo kwamba zimeshiriki timu nne bora za msimu uliopita lakini wao ndio mabingwa," amesema Kiemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live