KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wilfred Kidao amesema hali ya waamuzi kuboronga imewashtua mpaka wao baada ya matukio hayo kuongezeka. Alizungumza na Wandishi wa Habari leo Jumamosi kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya Shirikisho hilo, Kidao alisema wanatambua changamoto hiyo na tayari wameanza kuifanyia kazi. "Changamoto ipo hasa upande wa wasaidizi wanashindwa sana kutambua kuotea, lakini hilo linafanyiwa kazi," alisema. Kidao alisema makosa yanayofanyika sio Tanzania tu bali ni Afrika nzima wanakumbana na hali hiyo. "Ulaya tu sasa hivi ndio wametulia na matatizo kama haya baada ya uwepo wa VAR, lakini kwa Afrika changamoto ni kubwa mno na sio kwetu tu," alisema. "Tunajivunia Azam kwa kipindi hiki kwani wanatuonyesha matukio baada ya mchezo na hapo ndio tunaona, hii pia inafanya waamuzi wetu wazidi kuwa makini," alisema. Akizungumzia upande wa madai ya waamuzi kwenye mishahara yao, Kidao alisema wamekuwa wakijitahidi kufanya hivyo kwa ustadi mkubwa. "Kweli tunadaiwa na waamuzi na tumelipa raundi 12 bado raundi saba, hizo zilizobaki zitamaliziwa hivi karibuni kwa kuchukua pesa katika vyanzo vingine kwasababu pesa ya udhamini upande wa marefa huwa inaingia kwa awamu hivyo sisi tumejitahidi," alisema na kuongeza kwamba hata kama mtu anadai haamini mtu huyo kuharibu kazi yake.