Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichuya sasa kuibukia jeshini

Kichuya Qs Vita Kichuya sasa kuibukia jeshini

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa Namungo FC, Shiza Kichuya kuna asilimia kubwa pindi litakapofungwa dirisha dogo la usajili linaloendelea kwa sasa, akaibukia JKT Tanzania, inayonolewa na kocha Malale Hamsini.

Mwanaspoti limepata taarifa za ndani kutoka kwa mmoja wa kiongozi wa timu ya JKT Tanzania kwamba kila kitu kuhusiana na mchezaji huyo kinaenda sawa na muda wowote anaweza akasaini.

Japokuwa haijawekwa wazi ni mkataba wa muda gani ambao Kichuya alibakiza na Namungo, lakini inaelezwa taratibu zote zinafuatwa ili kuhakikisha wanainasa saini yake.

“Kichuya ni mchezaji mzuri na ana uwezo wa kutumia miguu miwili kucheza na ndio maana mwepesi wa kucheka na nyavu anapopata fursa hiyo,” alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

”Tunazungumza na viongozi wa Namungo kuona hilo jambo linakwenda kwa kuzingatia taratibu zinazotakiwa, ila ni asilimia kubwa winga huyo anaweza akajiunga na sisi.”

Kichuya alipata umarufu mkubwa baada ya kuichezea Simba miaka kadhaa iliyopita, kutokana na kiwango chake alichokuwa akikionyesha ikiwemo kuifunga Yanga, kama bahati aliyonayo straika wa KMC, Waziri Junior kuwafunga Wanamsimbazi mara nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live