Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichuya sasa anataka ndoo

Shiza Kichuya Mapinduzi Kichuya sasa anataka ndoo

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa Namungo, Shiza Kichuya amesema wanajisikia fahari kutimiza malengo waliyojipangia kama timu ya kufika nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi na sasa malengo yao ni kutwaa kombe hilo.

Kichuya alisema hayo wakati akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Aigle Noir ya Burundi ambapo Namungo walishinda 1-0 na kufikisha pointi nne hivyo kuongoza katika kundi D.

“Tunajisikia vizuri kufika hatua hii kwani tulijiandaa vizuri japokuwa timu nyingi zilijiandaa vizuri maana naona hata wakubwa nao wanapoteza mechi na kutolewa mapema sasa malengo yetu ni fainali na kuweza kutwaa kombe,” alisema Kichuya na kuongeza;

“Siri ya mafanikio yetu ni kumsikiliza kocha na kufanyia kazi nini ambacho anakitaka kwani kipindi cha kwanza tulikuja na plani yetu ikafeli wakati wa mapumziko tuliamua kubadili mbinu na hatimaye kufanikiwa na mimi kuibuka mchezaji bora wa mechi hiyo."

Aidha Kichuya alimtaja mchezaji aliyewapa shida Namungo kupenya ngome ya Aigle Noir kuwa ni Issa Ndikumana ambaye pia alitangazwa kuwa ni mchezaji mwenye nidhamu wa mchezo huo.

“Yule mchezaji aliyekuwa amevaa jezi namba 10 alitupa wakati mgumu kufika langoni kwao kwani ni mchezaji mzuri na timu nzima ya Aigle Noir wapo vizuri japokuwa tumewafunga,” alisema Kichuya.

Alisema kidogo alichokipata baada ya kutangazea mchezaji bora atagawana na wenzake kwani asingeweza kupata zawadi hiyo pasipo kuwa na ushirikiano na kucheza pamoja kama timu.

Namungo wanatarajia kushuka uwanjani kesho katika mchezo wao wa hatua ya nusu fainali ya kombe hilo dhidi ya Mlandege ambapo mshindi atacheza na Singida Big Stars.

Chanzo: Mwanaspoti