Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichuya kwenda mafunzo ya jeshi

Kichuya M(1) Kichuya kwenda mafunzo ya jeshi

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya JKT Tanzania huenda ikawakosa nyota zaidi ya Sita akiwemo Shiza Kichuya ambao wapo kwenye hatua za mwisho kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi kwa muda wa Miezi mitatu.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Malale Hamsin amethibitisha taarifa hizo nakubainisha kuwa benchi la ufundi limeweka Mpango Mkakati ili kufanya vizuri na kutoyumba bila kuwa na nyota hao.

Ikumbukwe kuwa Katika Mchezo dhidi ya Simba sc nyota sita wa Kikosi cha Kwanza walikua Wamenyoa Vipara tayari kwa Mafunzo. Nyota hao ni Pamoja na Shiza Kichuya, Martin Kigi, David Bryson, Wema Sadock, Hassan Nassoro, Maka Edward na Sixtus Sabilo.

Ndani ya miezi mitatu timu hiyo JKT Tanzania itakua na kibarua cha kuzitafuta alama tatu Kila Mchezo, dhidi ya Yanga SC, KMC, Kagera Sugar, Mashujaa, Tz Prisons, Tabora United, Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: