Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichuya ajiunga na Jeshi la Kujenga Taifa

Kichuya JKT Kichuya ajiunga na Jeshi la Kujenga Taifa

Wed, 1 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa JKT Tanzania, Shiza Kichuya kwa sasa ni askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT ) baada ya kufuzu mafunzo ya Jeshi hilo.

Klabu hiyo imetoa nafasi kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho kujiunga na Jeshi hilo kwa kuwapa mafunzo ya Kijeshi.

Katika pambano la JKT Tanzania dhidi ya Simba SC uliochezwa katika Uwanja wa Meja Isamuhyo Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho walionekana katika muonekano wa Vipara.

Kabla ya kwenda katika mafunzo hayo ya Kijeshi, wahusika huwa wananyolewa nywele na kubaki na Vipara tayari kwa kuanza mafunzo.

Miongoni mwa wachezaji wa kikosi hicho ambao waliopata mafunzo hayo ni Shiza Kichuya, Martin Kigi, David Bryson, Wema Sadock, Hassan Nassoro, Maka Edward, Sixtus Sabilo na Hassan Kapalata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live