Kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino alisema hajafurahishwa na kiwango cha timu yake katika Uwanja wa Stamford Bridge baada ya kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Brentford.
Chelsea imeshinda mechi moja dhidi ya Luton City kati ya 13 walizocheza uwanja wa nyumbani jambo ambalo Pochettino hakupendezwa. “Sina furaha. Wachezaji na klabu kwa jumla hawana raha kabisa,” Pochettino alikiambia kituo cha televisheni TNT Sports. “Ni muda mrefu sana tunahitaji kuwa imara tunapocheza nyumbani, nadhani natakiwa kufanyia kazi suala hili.”
Brentford imekuwa timu ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kushinda kila mechi kati ya mechi tatu za kwanza dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Hiyo inamaanisha kocha wa Brentford, Thomas Frank ameshinda mechi nyingi dhidi ya Chelsea katika Uwanja wa Stmford Bridge zaidi ya makocha wawili waliopita wa Chelsea (Graham Potter na Frank Lampard).
Kocha wa muda Lampard alishindwa kuipa Chelsea ushindi katika mechi tano walizocheza nyumbani msimu uliopita, huku Pochettino akiwa amecheza mechi moja uwanja wa nyumbani tangu alipoteuliwa.
Pochettino ameiongoza Chelsea kushinda nyumbani dhidi ya Wimbledon na Brighton kwenye Kombe la Carabao tu isipokuwa ligi.