Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichapo chamvuruga Alonso, aukubali mziki wa Atalanta

Xabi Alonso Bayer Leverkusen.jpeg Kocha wa Bayern Leverkusen, Xabi Alonso

Fri, 24 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Juzi usiku Atalanta ya Ligi Kuu ya Italia, Serie A iliibuka mabingwa wapya wa Europa League baada ya kuichapa Bayern Leverkusen mabao 3-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Aviva, ulioko Dublin, Ireland.

Kichapo hicho kinatokana na mabao ya Mnigeria Ademola Lookman aliyeipa Atalanta taji la kwanza kubwa la Ulaya kwa timu za Italia, tangu mara ya mwisho ifanye hivyo Parma mwaka 1999.

Ushindi huo pia umeivunja rekodi ya kutokufungwa katika mechi nyingi (51), ilizocheza Leverkusen na kumvuruga kocha wa mabingwa hao wa Bundesliga, Xabi Alonso huku akiukubali mziki wa Atalanta na kudai walikuja tofauti na wao walivyojiandaa.

Tangu kuanza kwa msimu huu Leverkusen imekuwa na kiwango bora kilichowawezesha kushinda Ligi Kuu Ujerumani na ilikuwa na nafasi ya kuchukua mataji matatu msimu huu kwani mbali ya Europa na Bundesliga pia imetinga fainali ya DFB-Pokal.

Ikiwa ingechukua mataji yote matatu na kuendeleza Unbeaten yao, timu hii ingeifikia rekodi ya Preston North End mwaka 1889 na ilichukua mataji matatu bila ya kupoteza mechi hata moja.

"Hatukupanga kufanya vibaya leo (jana), lakini ndiyo imeshatokea, hatukuweza kupambana na hali nyingi za mchezo kama tulivyojiandaa kwa sababu Atalanta walikuwa bora sana, rekodi yetu ya kutopoteza mechi imeharibiwa, niwape hongera Atalanta, walistahili kushinda."

Mfungaji wa mabao matatu yaliyoipa ubingwa Europa League Lookman ambaye aliwahi kupita Everton, Fulham na Leicester City za England alisema jana ilikuwa ni siku yake bora katika maisha yake ya soka, timu yake ilionyesha kiwango cha kushangaza.

"Tumeandika historia, tumefanikiwa."

Chanzo: Mwanaspoti