Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichapo cha Yanga chaivuruga Coastal, kuanika ukweli hadharani leo

Coastal Hadharani Leo Kichapo cha Yanga chaivuruga Coastal, kuanika ukweli hadharani leo

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya jana Novemba 9, kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga katika Uwanja wa CCM Mkwakwani.

Klabu ya Coastal Union wametangaza kuzungumza hadharani leo Novemba 9 kuanika ukweli wa wanachopitia.

Kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya Kijamii Coastal wameandika;

'Leo saa sita kamili mchana tutaanika Kila kitu,hakuna namna,tumechoka dharau na kejeli kwa klabu kubwa na kongwe kama sisi,unyonge sasa mwisho, tutazungumza na umma wa watanzania kupitia waandishi wa habari,karibuni sana ndugu wanahabari'.

Je unadhani Coastal kuna jambo gani wanalolipitia?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live