Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibwana mzuka umepanda

Kibwana Shomari Shhhoo Kibwana Shomari

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kufanya vizuri akiwa na Yanga, Oktoba kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Kibwana Shomari alitimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuichezea Taifa Stars.

Ilikuwa katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar kati ya Taifa Stars na Benin ambapo Kibwana alitimiza ndoto yake hiyo baada ya kuingia kipindi cha pili akitokea benchi kuchukua nafasi ya Israel Patrick na kukiwasha licha ya kwamba Stars ilipoteza kwa bao 1-0.

Baada ya mechi hiyo, Mwanaspoti lilipiga stori na Kibwana ambaye ameweka wazi kuwa alifurahi kutimiza ndoto yake na sasa ni kuifanyia kazi zaidi na kulipambania taifa.

“Siku nyingi nilikuwa nikitamani kuichezea timu yangu ya taifa, hapo awali nilicheza kwa timu za vijana na sasa ndoto kubwa ilikuwa kuichezea Taifa Stars na imetimia rasmi,” amesema Kibwana na kuongeza:

“Nashukuru benchi la ufundi kwa kunipa nafasi hii adhimu na sasa naanza kufanya kazi nma kupambana kuhakikisha nalipa heshima taifa langu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu katika nyakati tofauti.”

Hapo awali Kibwana hakuitwa kwenye kikosi hicho kinachonolewa na kocha Kim Poulsen lakini baada ya kuumia kwa Shomary Kapombe ambaye ni beki wa muda mrefu Taifa Stars, kibwana aliitwa kuziba pengo lake.

Kibwana kwa sasa yupo nchini Benin na Kikosi cha Taifa Stars wakijiandaa na mchezo wa marudiano Oktoba 10.

Chanzo: Mwanaspoti