Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibwana apata majeraha, ashindwa kuendelea na mchezo

Kibwana D Kibwana apata majeraha, ashindwa kuendelea na mchezo

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inawezekana Kibwana Shomary alitaka kuutumia mchezo wa jana dhidi ya Geita Gold kuonyesha kuwa bado ana uwezo wa kuendelea kuisaidia Yanga upande wa beki ya kulia lakini imekuwa bahati mbaya kwake baada ya kupata majeraha ambayo yamemfanya kushindwa kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kibwana ambaye amejikuta akipoteza namba mbele ya Yao Kouassi, jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara alipewa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza na kocha, Miguel Gamondi.

Nyota huyo akiwa na ari aliifanya Yanga kuwa na nguvu upande wake wa kulia ambako alikuwa akishirikiana na Stephane Azizi KI muda mwingine Augustine Okrah.

Akiwa katika harakati za kuifanya Yanga kupata bao kwenye mchezo huo, Kibwana alijikuta akichezewa vibaya mwishoni mwa kipindi cha pili na kushindwa kuendelea na mchezo.

Dakika kadhaa zilitumika na jopo la madaktari wa Yanga kwa ajili ya kumganga kisha akarejea uwanjani kwa dakika chache lakini nyota huyo alishindwa kuendelea na mchezo ikambidi Gamondi kufanya mabadiliko ya lazima kwa nafasi yake kuingia Yao.

Kibwana alisogea kwenye benchi la wachezaji wa akiba huku akichechemea kwa msaada wa madaktari huku akigugumia kwa maumivu na kuonekana kifundo chake cha mguu wa kulia kikifungwa bandeji nyeupe.

Wakati wa mapumziko nyota huyo alishindwa kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo huku akiwa na masikitiko wachezaji wenzake walienda kumpa moyo, ikiwa ni ishara ya wao nao kuguswa kwa kile ambacho mwenzao amekumbana nacho.

Kikosi cha Yanga; Djigui Diarra, Kibwana Shomary/ Yao Kouassi, Joyce Lomalisa, Gift Fred, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job/ Mudathir Yahya, Maxi Nzengeli, Stephane Azizi KI, Joseph Guede/ Clement Mzize, Kennedy Musonda/ Pacome Zouzoua na Augustine Okrah/ Skudu.

Geita Gold; Constantine Malimi, Mwaita Gereza, Anthony Mlingo, Hassan Mahamud, Kelvin Yondan , Samuel Onditi, Offen Chikola, Geofrey Julius, Valentino Mashaka, Tariq Seif.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: