Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibwana ajumuishwa Stars

Kibwana Pic Data Kibwana Shomari

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BEKI wa Yanga, Kibwana Shomari amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya Benin utakaopigwa Oktoba 07.

Awali kocha wa timu ya taifa, Kim Poulsen aliita kikosi cha nyota 25 huku jina la beki huyo likikosekana na sasa rasmi atakuwa miongoni wa wachezaji watakaoshuka katika dimba la Benjamin Mkapa.

Kibwana amekuwa katika kiwango bora ambapo katika msimu huu ametumika kwenye safu ya ulinzi upande wa kushoto ndani ya klabu ya Yanga.

Akizungumzia kuitwa kwa beki huyo, Ofisa Habari wa Yanga, Hassn Bumbuli amesema ni kweli wepokea ombi la mchezaji huyo kujiunga na Stars na mchezaji muda wowote kuanzia sasa atajiunga na wenzake.

"Tumepokea taarifa ya wito wa Kibwana. Na kwa heshima tumemruhusu akajiunge na timu ya Taifa wakati tukisubiri barua rasmi kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambayo tutaipata Jumatatu, Tunajivunia kuitwa kwake na tunampongeza sana, tunaamini kocha hakufanya makosa katika uteuzi wake kwani ameona kuna kitu kwa kijana wetu," amesema Bumbuli

Kibwana amezitumikia timu zote za Taifa kuanzia ngazi ya vijana U17 na U20 anaungana na Ramadhani Kabwili, Feisal Salum, Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job ambao walijumuishwa katika kikosi kilichotangazwa wiki iliyopita.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz