Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibwana Shomari aamua kurejea kwao

Kibwana 4 WA0010 Kibwana Shomari

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki nyota wa timu ya Yanga Kibwana Shomari, baada ya Ligi kusimama kupisha michezo ya kirafiki ya timu ya taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ametumia mwaya huo kurejea nyumbani kwao Morogoro na kuwatembelea watu mbali mbali waliofanikisha mafaniko yake ya Soka.

Kibwana Mkazi wa Kichangani Manispaa ya Morogoro aliyejenga Mjengo wake Kihonda, Mwanzo mwa wiki hii alitinga Uwanja wa Saba saba kuisapoti timu yake ya Moro Kids iliyotinga fainali Michuano ya Azam Sports Federation Cup 2023-24.

Mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo Kibwana aliyeketi nyuma ya benchi la Moro Kids kwa muda wote wa dakika 90 alizungumza na Viongozi wa timu ya Moro Kids Mratibu Mkuu Rajab Kindagule, na Meneja Mussa Miraji.

Kama hiyo haitoshi baada ya kuzungumza na Viongozi hao Kibwana alipanda jukwaani na kuzungumza kwa muda mrefu na kocha wa Moro kids anayefunisha watoto chini ya miaka 10 Ticha Majuto ambayendiye aliyeibua kipaji cha Kibwana toka akiwa na umri wa miaka 10.

Kibwana baada ya kuonyesha kipaji kwenye Taasisi hiyo ya Moro Kids inayoongoza nchini kwa kuzalisha wachezaji wengi wanaong’ara kwa sasa Ligi Kuu ya Tanzania Bara alijiungana na Mtibwa B.

Kama hiyo haitoshi beki huyo wa kulia baada ya kuonyeha kiwango kizuri Uongozi wa Mtibwa ulimpandisha timu ya wakubwa inayoshiriki Ligi kuu.

Huko nako aliendelea kuonyesha kiwango bora kilichowavutia Viongozi wa Yanga walioamua kumsajiri akiitumikia timu hiyo yenye maskani yake Kariakoo Makutano ya Mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wachezaji nyota wanaotamba kwa sasa ligi kuu walioibuliwa na kituo hicho cha Moro Kids ni pamoja na Kibwana Shomari, Nikson Kibabage, Diksoni Job na Kipa Abuutwalibu Msheri wote wanakipiga Yanga.

Wengine ni Mzamiru Yassin’Simba’ Shiza Kichuya’Namungu’ Hamad Waziri’Kuku’ Singida Fouantain Gate.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live