Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibwana, Mshery wanasepa Yanga?

Kibwanaaa W2 C.jpeg Kibwana, Mshery wanasepa Yanga?

Sun, 30 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa Yanga Abdutwalib Mshery na beki wa kulia Kibwana Shomari wamemaliza mikataba yao na wapo huru kujiunga na timu yoyote kama mazungumzo na uongozi wa Yanga Sc hayatakamilika.

Msimamizi wa wachezaji hao, George Job amesema wachezaji hao wameshamaliza mikataba yao na bado wanaangalia ofa kutoka timu nyingine mbalimbali zilizoomba huduma yao ingawa mazungumzo na Yanga ambayo imeonesha nia ya kuwabakiza ,bado yanaendelea.

“Kwa sasa wachezaji hao Kibwana na Msheri, wapo huru na wamepata ofa kutoka timu nyingi za ndani lakini Yanga wameonyesha nia ya kuwabakiza wachezaji hao na leo (jana) tulikuwa katika mazungumzo nao ingawa bado hayajakamilika,” ameeleza George Job.

Alisema mazungumzo hayo yalishindwa kufanyika mapema kwa sababu Yanga ilikuwa katika masuala ya kufungiwa kusajili wachezaji wa ndani na nje kutokana na madai ambayo hadi sasa wameshamalizana nayo na wapo huru kusajili ndiyo maana mazungumzo yameanza sasa.

George amesema Msheri kwa sasa yupo mapumzikoni kwa kuwa baada ya wachezaji kupewa mapumziko yeye alikuwa na timu ya taifa kule Zambia lakini pia aliporudi aliendelea kucheza katika mabonanza mbalimbali ya mechi za hisani yaliyoandaliwa na wachezaji wenzake hivyo hakupata muda mzuri wa kupumzika kama wenzake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live