Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibuta kuanza na Geita, muda wapanguliwa

Mwanauta Kibuta kuanza na Geita, muda wapanguliwa

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mchezaji Mwana Kibuta, hatimaye anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza katika timu ya Dodoma Jiji dhidi ya Geita Gold kesho Alhamisi, baada ya kupata kibali cha kazi, kiongozi wa juu wa timu hiyo amethibitisha.

Kiungo huyo kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pamoja na mwenzake Randy Bangala ndio wachezaji pekee ambao walikua bado hawajapata vibali vya kuwawezesha kucheza mechi za timu hiyo, tangu waliposajiliwa.

Randy ambaye ni mdogo wa Yannick Bangala wa Yanga, atalazimika kusubiri hadi mchezo ujao dhidi ya Simba ili kujua hatma ya kucheza endapo kibali chake kitakamilika, ila kwa Kibuta ni rasmi ameshapata na mchezo wa Geita kesho atacheza.

Mchezo baina ya Dodoma Jiji na Geita umelazimika kubadilishwa muda mara mbili, awali ulikuwa uchezwe majira ya saa 1 jioni katika uwanja wa Jamhuri, ukabadilishwa uwanja kuwa Liti muda wa saa 10 jioni na sasa umewekwa saa nane mchana.

Kutofunguliwa kwa uwanja wa Jamhuri ambao una siku 10 tangu ukaguliwe, lakini imeshindikana kufunguliwa na kufanya timu ya Dodoma Jiji kubaki kuchezea Liti Singida, kumalizia mchezo huo dhidi ya Geita.

Timu zote mbili hazijashinda mchezo katika ligi, Geita wakiwa na sare tatu wakipoteza mchezo mmoja, Dodoma Jiji wakiwa na sare mbili na kupoteza mechi mbili.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz