Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kibu yuko Ulaya, ninawadai Simba - Meneja Carlos

Kibu 2026 Kibu yuko Ulaya, ninawadai Simba - Meneja Carlos

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa kiungo mshambuliaji wa Simba Sc, Kibu Dennis, Carlos amefichua kuwa mchezaji huyo yupo Ulaya licha ya kuwa amelipwa stahiki zake zote na haidai Simba Sc chochote.

Kauli hiyo ya Carlos inakuja huku kukiwa na sintofahamu kuhusu mchezaji huyo ambaye mpaka sasa hajafika kambini licha ya timu yake kuingia kambini wiki tatu zilizopita nchini Misri.

Carlos akibainisha kuwa yeye binafsi (Meneja ) anaidai Simba ‘agency fee’ ya usajili wa Zimbwe Jr na Hussein Kazi ila kwa suala la Kibu mwenye mamlaka ya kuliongelea ni simba

Hata hivyo Carlos hajaweka bayana kuwa Kibu yupo Nchi gani huko Ulaya lakini maelezo yake yanaashiria nyota huyo yupo ulaya kwa ajili ya majaribio.

Aidha Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally amesema hana taarifa za nyota huyo kuwa Ulaya na kwamba yeye anachojua Kibu yupo Kigoma huku akiongeza kuwa mwenye nafasi nzuri ya kuzungumzia sababu za Kibu kutokwepo kambini ni mchezaji mwenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live